sw_act_text_ulb/09/13.txt

2 lines
507 B
Plaintext

\v 13 Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia kutoka kwa wengi kuhusu mtu huyu, kwa kiasi gani amewafanyia mabaya watu wako watakatifu walioko Yerusalemu; \v 14 Anayo mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kuweka katika vifungo kila mtu
hapa anayeliitia jina lako." \v 15 Lakini Bwana akamwambia, "Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, kulibeba jina langu mbele ya watu wa Mataifa na wafalme na wana wa Israeli. \v 16 Kwa maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu".