sw_act_text_ulb/08/26.txt

1 line
460 B
Plaintext

\v 26 Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, "Amka na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza." ( Njia hii iko katika jangwa). \v 27 Akaamka na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya Kandasa; malkia wa Waethiopia. Ndiye aliyekuwa msimamizi wa hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu. \v 28 Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma Kitabu cha nabii Isaya.