sw_act_text_ulb/08/09.txt

1 line
411 B
Plaintext

\v 9 Lakini palikuwepo na mtu fulani katika mji ule aliyeitwa Simon, ambaye hapo awali alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu. \v 10 Wasamaria wote kutoka mdogo hadi mkubwa, walimwangalia kwa makini; wakasema;"mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu." \v 11 Wakamsikiliza kwa maana aliwashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.