sw_act_text_ulb/08/01.txt

1 line
427 B
Plaintext

\c 8 \v 1 Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. Ndipo siku hio yakaanza mateso makuu kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote walitawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume. \v 2 Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake. \v 3 Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwavuta nje wanawake na waume, na kuwatupa gerezani.