1 line
477 B
Plaintext
1 line
477 B
Plaintext
\v 35 Kisha akawaambia, "Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa. \v 36 Kwa sababu, zamani zilizopita, Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu, na idadi ya watu, wapata mia nne walijiunga naye. Aliuawa, na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika na kuwa si kitu. \v 37 Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake. Naye pia aliangamia na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika. |