sw_act_text_ulb/08/14.txt

1 line
410 B
Plaintext

\v 14 Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa sasa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma kwao Petro na Yohana. \v 15 Wakati walipokuwa wakishuka waliwaombea kwamba, wampokee Roho Mtakatifu. \v 16 Kwani mpaka wakati huo Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata Mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu. \v 17 Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu.