sw_act_text_ulb/21/27.txt

1 line
532 B
Plaintext

\v 27 Siku hizo saba zilipokaribia kumalizika, baadhi ya Wayahudi kutoka Asia wakamuona Paulo Hekaluni, na makutano wakakasirika, na wakamnyoshea mikono. \v 28 Walikuwa wanapiga kelele, "Watu wa Israeli, tusaidieni. Huyu ni yule mtu ambaye hufundisha watu kila mahali mambo ambayo ni kinyume na watu, sheria, na mahali hapa. Pia amewaleta Wayunani katika Hekalu na kupanajisi mahali hapa patakatifu." \v 29 Kwa kuwa hapo kabla walikuwa wamemwona Trofimo Muefeso akiwa pamoja naye mjini, nao walidhani kwamba Paulo alimleta hekaluni.