sw_act_text_ulb/02/46.txt

1 line
285 B
Plaintext

\v 46 Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu. Pia walimega mkate kwa nyumba zao, na walishiriki chakula kwa furaha na ukarimu wa mioyo, \v 47 wakimsifu Mungu na kuwa na kibali na watu wote, na Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.