sw_act_text_ulb/28/16.txt

1 line
565 B
Plaintext

\v 16 Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda. \v 17 Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale wanume waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, "Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi. \v 18 Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo.