sw_act_text_ulb/01/06.txt

1 line
401 B
Plaintext

\v 6 Na walipokuwa wamekutanika pamoja walimuuliza, "Bwana, je, huu ndio muda utakaowarudishia Israeli ufalme?" \v 7 Yeye akawaambia, "Siyo sawa kwenu kujua wakati au majira ambayo Baba amekusudia kwa mamlaka yake mwenyewe." \v 8 Lakini mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu kote katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria mpaka mwisho wa dunia."