sw_act_text_ulb/20/01.txt

1 line
416 B
Plaintext

\c 20 \v 1 Baada ya ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi na baada ya kuwatia moyo, aliwaaga na akaondoka kwenda Makedonia. \v 2 Naye akiishakupita mikoa hiyo na alikuwa akiwatia moyo waumini, akaingia Uyunani. \v 3 Baada ya yeye kuwa pale kwa muda wa miezi mitatu, njama ziliundwa dhidi yake na Wayahudi alipokuwa akikaribia kusafiri kwa njia ya bahari kuelekea Shamu, hivyo aliazimu kurudi kupitia Makedonia.