sw_act_text_ulb/11/11.txt

1 line
506 B
Plaintext

\v 11 "Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; walikuwa wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu. \v 12 Roho akaniamuru niende pamoja nao, na nisitofautiane nao. Hawa ndugu sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu yule. \v 13 Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, 'Watume watu Yafa wakamlete simoni ambaye jina lake lingine ni Petro. \v 14 Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote.'