sw_act_text_ulb/11/07.txt

1 line
371 B
Plaintext

\v 7 Kisha nikasikia sauti ikisema nami, 'Amka, Petro, chinja na ule!' \v 8 Nikasema, 'Siyo hivyo, Bwana, kwa maana mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu' \v 9 Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, 'kile ambacho Mungu amekitakasa, usikiite najisi'. \v 10 Hii ilitokea mara tatu, na kisha kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.