sw_act_text_ulb/25/23.txt

1 line
415 B
Plaintext

\v 23 Hivyo kesho yake, Agripa na Bernike walifika na shamrashamra nyingi; walifika katika ukumbi na maafisa wa kijeshi, na watu mashuhuri wa mji. Na Festo alipotoa amri, Paulo aliletwa kwao. \v 24 Festo akasema, "Mfalme Agripa, na watu wote ambao wapo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu; jumuiya yote ya Wayahudi walikata rufaa kwangu huko Yerusalemu na hapa pia, na wakapiga kelele kwangu kwamba asipate kuishi.