sw_act_text_ulb/20/17.txt

1 line
587 B
Plaintext

\v 17 Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa. \v 18 Walipofika kwake, akawaambia, ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote. \v 19 Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi. \v 20 Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu kitu chochote ambacho kilikuwa muhimu, na jinsi mimi nilivyowafundisha wazi wazi na pia kwenda nyumba kwa nyumba. \v 21 Nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu.