sw_act_text_ulb/18/24.txt

1 line
490 B
Plaintext

\v 24 Sasa Myahudi mmoja aitwaye Apolo, aliyezaliwa huko Alexandria, alikuja Efeso. Alikuwa na ufasaha katika kuongea na hodari katika Maandiko. \v 25 Apollo alikuwa ameelekezwa katika mafundisho ya Bwana. Akiwa na bidii katika roho, aliongea na kufundisha kwa usahihi mambo yanayomuhusu Yesu, ila alijua tu ubatizo wa Yohana. \v 26 Apolo akaanza kuzungumza kwa ujasiri katika hekalu. Lakini Prisila na Akwila walipomsikia, walimchukua kando na wakumwelezea njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.