sw_act_text_ulb/13/42.txt

1 line
284 B
Plaintext

\v 42 Wakati Paulo na Barnaba wakiondoka, watu wakawaomba waongee maneno haya siku ya Sabato iliyofuata. \v 43 Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha, Wayahudi wengi na waongofu thabiti waliwafuata Paulo na Barnaba, ambao waliongea nao na waliwahimiza waendelee katika neema ya Mungu.