sw_act_text_ulb/13/01.txt

1 line
455 B
Plaintext

\c 13 \v 1 Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri), Lukio wa Kirene, Manaeni( ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli. \v 2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, "Nitengeeni pembeni Barnaba na Sauli, kuifanya kazi ambayo nimewaitia." \v 3 Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende zao.