sw_act_text_ulb/04/01.txt

1 line
471 B
Plaintext

\c 4 \v 1 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakizungumza na watu, makuhani na nahodha wa hekalu na masadukayo waliwajia. \v 2 Walikuwa wameudhika sana kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wanafundisha watu na kutangaza katika Yesu ufufuo kutoka kwa wafu. \v 3 Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni. \v 4 Lakini watu wengi waliokuwa wamesikia ujumbe waliamini; na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini walikuwa kama elfu tano.