sw_act_text_ulb/01/12.txt

1 line
485 B
Plaintext

\v 12 Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima ambao unaitwa wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, kiasi cha umbali wa kutembea mwendo wa Sabato. \v 13 Walipofika walikwenda ghorofani walikokuwa wakikaa. Nao ni Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Thomaso, Batholomayo, Mathayo, Yakobo Mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda Mwana wa Yakobo. \v 14 Wote walikuwa wamejitolea kwa nia moja kuomba, miongoni mwao walikuwemo wanawake, na Mariamu Mama yake Yesu, na kaka zake.