\v 22 Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. \v 23 Waliandika hivi kwa mikono yao, "Kutoka kwa mitume, wazee na ndugu, kwa ndugu wa Mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu!