\v 20 Lakini Petro akamwambia; fedha yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu umefikiri kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa. \v 21 Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu. \v 22 Hivyo basi, tubu uovu wako huu na kumwomba Bwana anawenza labda kukusamehe nia ya moyo wako. \v 23 Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi."