\v 3 Muda wa saa tisa za mchana, aliona wazi katika maono Malaika wa Mungu akija kwake. Malaika akamwambia "Kornelio!" \v 4 Kornelio akatazama malaika na akaogopa sana akasema, "kuna nini bwana?" Malaika akamwambia "Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu". \v 5 Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro. \v 6 Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari."