sw_act_text_reg/24/10.txt

1 line
504 B
Plaintext

\v 10 Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, "Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako. \v 11 Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu. \v 12 Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji; \v 13 na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.