sw_act_text_reg/22/22.txt

1 line
388 B
Plaintext

\v 22 Watu wakamruhusu aongee juu ya neno hili. Lakini baadaye walipaza sauti na kusema, "mwondoe mtu huyu katika nchi: kwa sababu sio sahihi aishi." \v 23 Walipokuwa wakipaza sauti, na kutupa mavazi yao na kutupa mavumbi juu, \v 24 jemedari mkuu akaamuru Paulo aletwe ngomeni. Akaamuru aulizwe huku anapigwa mijeledi, ili yeye mwenyewe ajue kwa nini walikuwa wanampigia kelele namna ile.