sw_act_text_reg/06/02.txt

1 line
355 B
Plaintext

\v 2 Mitume kumi na wawili waliwaita kusanyiko lote la wanafunzi na kusema, "Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu na kuhudumia mezani. \v 3 Kwa hiyo, ndugu, chagueni, wanaume saba, kutoka miongoni mwenu, watu wema, waliojaa Roho na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi huduma hii. \v 4 Na sisi, tutaendelea daima katika kuomba na katika huduma ya neno."