sw_act_text_reg/27/07.txt

1 line
368 B
Plaintext

\v 7 Baada ya kuwa tumesafiri polepole kwa siku nyingi na hatimaye tukawa tumefika kwa taabu karibu na Kinidas, upepo haukuturuhusu tena kuelekea njia hiyo, hivyo tukasafiri kandokando ya kivuli cha Krete tukiukinga upepo, mkabala na Salmone. \v 8 Tukasafiri kandokando ya pwani kwa ugumu, mpaka tukafika mahali palipoitwa Fari Haveni ambayo iko karibu na mji wa Lasi.