sw_act_text_reg/10/13.txt

1 line
348 B
Plaintext

\v 13 Tena sauti ikasema kwake "Amka, Petro chinja na ule". \v 14 Lakini Petro akasema "Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu. \v 15 Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili "Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu". \v 16 Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.