sw_act_text_reg/04/08.txt

1 line
473 B
Plaintext

\v 8 Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akawaambia, "Ninyi wakuu wa watu, na wazee, \v 9 kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa - kwa namna gani mtu huyu alifanywa mzima? \v 10 Hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel, kwamba kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye mlimsulibisha, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, ni kwa njia yake kwamba mtu huyu anasimama hapa mbele yenu akiwa mwenye afya.