sw_act_text_reg/04/01.txt

1 line
488 B
Plaintext

\v 1 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakizungumza na watu, makuhani na mlinzi wa hekalu na masadukayo waliwaendea. \v 2 Walikuwa wameudhika sana kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wanawafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. \v 3 Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni. \v 4 Lakini watu wengi waliokuwa wamesikia ujumbe waliamini; na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini walikadiliwa kuwa elfu tano.