sw_act_text_reg/01/09.txt

1 line
427 B
Plaintext

\v 9 Bwana Yesu alipokwisha yasema haya, wakiwa wanatazama juu, Yeye aliinuliwa juu, na wingu likamfunika wasimwone kwa macho yao. \v 10 Wakati wanatazama mbinguni kwa makini akienda, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi meupe. \v 11 Walisema, "Enyi watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama hapa mkitazama mbinguni?" Huyu Yesu aliyepaa juu mbinguni atarudi kwa namna ile ile kama mlivyomuona akienda mbinguni.