sw_act_text_reg/21/34.txt

1 line
368 B
Plaintext

\v 34 Baadhi ya watu kwenye umati walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kingine. Kwa kuwa jemadari hakuweza kuwaambia chochote kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo aletwe ndani ya ngome. \v 35 Basi alipofika kwenye ngazi, akachukuliwa na askari kwa sababu ya ghasia za umati. \v 36 Maana umati wa watu walimfuata na waliendelea kupiga kelele, "Mwondoeni huyu!"