sw_act_text_reg/21/22.txt

1 line
401 B
Plaintext

\v 22 Tunapaswa tufanye nini? Bila shaka watasikia kwamba wewe umekuja. \v 23 Hivyo fanya kile sisi tunachokuambia sasa: tunao watu wanne ambao wameweka nadhiri. \v 24 Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao, na uwalipie gharama zao, ili waweze kunyoa vichwa vyao. Hivyo kila mmoja apate kujua kwamba mambo waliyoambiwa kuhusu wewe ni ya uongo. Watajifunza kwamba wewe pia unafuata sheria.