sw_act_text_reg/19/15.txt

1 line
390 B
Plaintext

\v 15 Roho wachafu wakawajibu, "Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? " \v 16 Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa. \v 17 Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.