sw_act_text_reg/02/08.txt

1 line
410 B
Plaintext

\v 8 Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo? \v 9 Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia, \v 10 katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi, \v 11 Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu."