sw_act_text_reg/02/01.txt

1 line
387 B
Plaintext

\v 1 Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja. \v 2 Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. \v 3 Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao. \v 4 Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema.