sw_2ti_text_ulb/01/08.txt

1 line
605 B
Plaintext

\v 8 Kwa hiyo usiuonee haya ushuhuda kuhusu Bwana wetu, wala wangu mimi Paulo mfungwa wake, Bali ushiriki mateso kwa ajili ya Injili ,sawasawa na uweza wa Mungu. \v 9 Ni Mungu aliyetuokoa na kutuita kwa wito mtakatifu. Hakufanya hivi kulingana na kazi zetu bali kulingana na neema na mpango wake mwenyewe, Alitupatia mambo haya katika Kristo Yesu kabla ya nyakati kuanza. \v 10 Lakini sasa wokovu wa Mungu umekwishafunuliwa kwa kuja kwa mwokozi wetu Kristo Yesu, Ni Kristo aliyeikomesha mauti na kuleta uzima usiokoma kwa nuru ya Injili. \v 11 Kwa sababu hiyo nilichaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu.