Thu Mar 17 2022 09:18:47 GMT+0200 (South Africa Standard Time)

This commit is contained in:
Tomussone José Machinga 2022-03-17 09:18:48 +02:00
commit b64bf2308f
21 changed files with 87 additions and 0 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Paulo, Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. \v 2 Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

1
01/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu. Maana hivi ndivyo itupasavyo, kwa kuwa imani yenu inakua sana, na upendo wenu kwa kila mtu uongezeke mwingi. \v 4 Hivyo sisi wenyewe tunaongea kwa fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu. Tunazungumza habari ya saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote. Tunaongea kwa habari ya mateso mnayostahimili. \v 5 Hii ndiyo ishara ya hukumu ya haki ya Mungu. Matokeo ya haya ni kuwa ninyi mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu ambao kwa ajili yake mnateswa.

1
01/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Kwa kuwa ni haki kwa Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi, \v 7 na kuwapa raha ninyi mteswao pamoja nasi. Atafanya hivi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake. \v 8 Katika mwali wa moto atawalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu.

1
01/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Watateseka kwa maangamizi ya milele wakiwa wametengwa na uwepo wa Bwana na utukufu wa nguvu zake. \v 10 Atafanya wakati atakapokuja ili kutukuzwa na watu wake na kustaajabishwa na wote walioamini. Kwa sababu ushuhuda wetu kwenu ulisadikiwa kwenu.

1
01/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kwa sababu hii twawaombea ninyi siku zote. Twaomba kwamba Mungu wetu awahesabu kuwa mlistahili kuitwa. Twaomba kwamba apate kutimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu. \v 12 Tunaomba mambo haya ili mpate kulitukuza jina la Bwana Yesu. Tunaomba kwamba mpate kutukuzwa naye, kwa sababu ya neema ya Mungu na ya Bwana Yesu Kristo.

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Sasa kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa pamoja ili tuwe naye: tunawaomba ninyi ndugu zetu, \v 2 kwamba msisumbuliwe wala kutabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonkana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja.

1
02/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Mtu na asiwadanganye kwa namna yoyote. Kwa kuwa haitakuja mpaka lile anguko litokee kwanza na mtu wa uasi afunuliwe, yule mwana wa uharibifu. \v 4 Huyu ndiye apingaye naye hujiinua mwenyewe akimpinga Mungu na chochote kinachoabudiwa. Na matokeo yake, hukaa kwenye hekalu la Mungu na kujionyesha yeye kuwa kama Mungu.

1
02/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa nanyi niliwaambia juu ya mambo haya? \v 6 Sasa mnajua kile kinachomzuia, ili kwamba aweze kufunuliwa kwa wakati sahihi utakapowadia. \v 7 Kwa kuwa siri ya yule mtu mwenye kuasi inafanya kazi mpaka sasa, ila tu kuna anaye mzuia sasa mpaka atakapotolewa njiani.

1
02/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Ndipo yule mwenye kuasi atakapofunuliwa, amabaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake. Bwana atamfanya kuwa si chochote kwa ufunuo wa ujio wake. \v 9 Ujio wa yule mwenye kuasi utakuwa kwa sababu ya kazi ya shetani kwa nguvu zote, ishara na maajabu ya uongo, \v 10 na uongo wote wenye udhalimu. Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea, kwa sababu hawakuupokea upendo wa kweli kwa ajili ya kuokolewa kwao.

1
02/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kwa sababu hiyo Mungu anawatumia kazi yenye uovu ili waamini uongo. \v 12 Matokeo yake ni kwamba wote watahukumiwa, wale ambao hawakuamini ukweli bali wao hujifurahisha katika udhalimu.

1
02/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli. \v 14 Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. \v 15 Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu.

1
02/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema, \v 17 awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema.

1
03/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu. \v 2 Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani. \v 3 Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.

1
03/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza. \v 5 Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.

1
03/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu. \v 7 Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu. \v 8 Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi. \v 9 Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.

1
03/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, "Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile." \v 11 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. \v 12 Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

1
03/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi. \v 14 Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika. \v 15 Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu.

1
03/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote. \v 17 Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo. \v 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.

39
LICENSE.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,39 @@
## Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International
### Human-Readable Summary
The Creative Commons Attribution-Share Alike 4.0 International License is available at
http://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0/.
#### This is a human-readable summary of (and not a substitute for) the License.
### You are free to:
* **Share** — copy and redistribute the material in any medium or format.
* **Adapt** — remix, transform, and build upon the material for any purpose, even commercially.
The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms.
### Under the following terms:
* **Attribution** —You must give appropriate credit, provide a link to the license, and indicate if changes were made. You may do so in any reasonable manner, but not in any way that suggests the licensor endorses you or your use.
* **ShareAlike** — If you remix, transform, or build upon the material, you must distribute your contributions under the same license as the original.
* **No additional restrictions** — You may not apply legal terms or technological measures that legally restrict others from doing anything the license permits.
### Notices:
* You do not have to comply with the license for elements of the material in the public domain or where your use is permitted by an applicable exception or limitation.
* No warranties are given. The license may not give you all of the permissions necessary for your intended use. For example, other rights such as publicity, privacy, or moral rights may limit how you use the material.
This PDF was generated using Prince (https://www.princexml.com/).

1
front/title.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
2 Wathesalonike

29
manifest.json Normal file
View File

@ -0,0 +1,29 @@
{
"package_version": 6,
"format": "usfm",
"generator": {
"name": "ts-desktop",
"build": "27"
},
"target_language": {
"id": "sw",
"name": "Kiswahili",
"direction": "ltr"
},
"project": {
"id": "2th",
"name": "2 Thessalonians"
},
"type": {
"id": "text",
"name": "Text"
},
"resource": {
"id": "reg",
"name": "Regular"
},
"source_translations": [],
"parent_draft": {},
"translators": [],
"finished_chunks": []
}