sw_2sa_text_reg/14/32.txt

1 line
428 B
Plaintext

\v 32 Absalomu akamjibu Yoabu, "Tazama nilituma neno kwako kusema, 'Njoo ili nikutume kwa mfalme kusema, "Kwa nini nilikuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningesalia huko. Kwa hivyo sasa niache niuone uso wa mfalme na kama nina hatia basi na aniue." \v 33 Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi ardhini mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.