sw_2sa_text_reg/12/19.txt

1 line
389 B
Plaintext

\v 19 Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, "Je mtoto amekufa?" Wakajibu, "Amekufa." \v 20 Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudi katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala.