sw_2sa_text_reg/03/22.txt

1 line
383 B
Plaintext

\v 22 Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani. \v 23 Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, "Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani."