sw_2sa_text_reg/12/11.txt

1 line
458 B
Plaintext

\v 11 Yahwe asema, 'Tazama, nitaleta maafa dhidi yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe. Nitachukua wake zako, mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako wakati wa mchana. \v 12 Kwa maana wewe ulitenda dhambi hii sirini, lakini mimi nitatenda jambo hili wakati wa mchana mbele za Israeli wote. \v 13 Ndipo Daudi alipomwambia Nathani, "Nimemtenda dhambi Yahwe." Nathani akamjibu Daudi, "Yahwe naye ameiachilia dhambi yako. Hautakufa.