sw_2sa_text_reg/12/04.txt

1 line
524 B
Plaintext

\v 4 Siku moja tajiri akapata mgeni, lakini yeye hakuwa tiyari kuchukua mnyama kutoka katika kundi lake la ng'ombe au kundi la kondoo ili kumwandalia chakula. Badala yake alichukua mwanakondoo wa masikini na akampika kwa ajili ya mgeni wake. \v 5 Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, "Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa. \v 6 Ni lazima alipe mwanakondoo mara nne zaidi kwa ajili ya kile alichokifanya, na kwa sababu hakuwa na huruma kwa mtu maskini.