sw_2sa_text_reg/05/19.txt

1 line
480 B
Plaintext

\v 19 Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, "Je niwashambulie wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?" Yahwe akamwambia Daudi, "Washambulia, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya wafilisti." \v 20 Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu. \v 21 Wafilisiti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.