sw_2sa_text_reg/07/24.txt

1 line
374 B
Plaintext

\v 24 Umeiimarisha Israel kama watu wako daima, na wewe, Yahwe, kuwa Mungu wao. \v 25 Basi sasa, Yahwe Mungu, ahadi uliyofanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima. Ufanye kama ulivyo sema. \v 26 Na jina lako liwe kuu daima, ili watu waseme, 'Yahwe wa majeshi ni Mungu wa Israeli,' wakati nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako itakapokaa imara mbele zako daima.