sw_2sa_text_reg/24/15.txt

1 line
441 B
Plaintext

\v 15 Hivyo akatuma tauni juu ya Israeli kuanzia asubuhi kwa muda ulioamriwa, na watu sabini na tano elfu kutoka Dani mpaka Beersheba wakafa. \v 16 Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, "Yatosha! Rudisha mkono wako sasa." Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.