sw_2sa_text_reg/04/01.txt

1 line
456 B
Plaintext

\v 1 Ikawa Ishboshethi, mwana wa Sauli, aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, mikono yake ikadhoofika, na Israeli yote ikataabika. \v 2 Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi vya askari. Mmoja wao alikuwa Baana na mwingine alikuwa Rekabu, wana wa Rimoni Mbeerothi wa wana wa Benjamini(kwa maana Berothi ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini, \v 3 na Waberothi walikimbilia Gitaimu na wamekuwa wakiishi pale hadi sasa).