sw_2sa_text_reg/03/24.txt

1 line
398 B
Plaintext

\v 24 Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, "Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye ameenda? \v 25 Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?" \v 26 Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sira, lakini Daudi hakulijua hili.