sw_2sa_text_reg/13/34.txt

1 line
413 B
Plaintext

\v 34 Absalomu akakimbia. Mtumishi aliyekuwa akiangalia akainua macho yake na kuona watu wengi wakija njiani kando ya kilima upande wake wa magharibi. \v 35 Kisha Yehonadabu akamwambia mfalme, "Tazama, wana wa mfalme wanakuja. kama mtumishi wako alivyosema." \v 36 Ikawa mara alipomaliza kusema wana wa mfalme wakafika, wakainua sauti zao na kulia. Na mfalme pamoja na watumishi wake wote pia wakalia kwa uchungu.