sw_2sa_text_reg/13/05.txt

1 line
476 B
Plaintext

\v 5 Ndipo Yehonadabu akamwambia, "Lala kitandani mwako na ujifanye kuwa mgonjwa. Wakati baba yako atakapo kuja kukuona, mwambie, Tafadhali mtume dada yangu Tamari aandae chakula mbele yangu, ili kwamba nikione na kula kutoka mkononi mwake?" \v 6 Hivyo Amnoni akalala na kujifanya kuwa mgonjwa. Mfalme alipokuja kumwona, Amnoni akamwambia mfalme, "Tafadhari mtume Tamari dada yangu aandae chakula kwa ajili ya ugonjwa wangu mbele yangu ili kwamba nikile kutoka mkononi mwake."